Jua namna tafsiri zetu zinavyoundwa
Tafsiri Google ni nini?
Google Tafsiri ni huduma isiyokuwa na malipo ya kutafsiri ambayo hutoa tafsiri za papo hapo kati ya lugha nyingi tofauti. Inaweza kutafsiri maneno, sentensi na kurasa za wavuti kati ya jozi zozote za lugha zinzowezakutumika. Kupitia Google Tafsiri, tunatumaini kufanya maarifa yapatikane kwa wote na yawe ya maana, bila kujali lugha yaliyoandikiwa.
Inafanya kazi aje?
Wakati Google Tafsiri inapozalisha utafsiri, hutafuta ruwaza katika mamia ya mamilioni ya nyaraka ili kusaidia kuamua utafsiri bora kwa ajili yako. Kwa kugundua ruwaza katika nyaraka ambazo tayari zimetafsiriwa na watafsiri wanadamu, Google Tafsiri inaweza kukisia kwa werevu utafsiri ambao unafaa. Mchakato huu wa kutafuta ruwaza katika viwango vikubwa vya maandishi huitwa "utafsiri wa mashine ya takwimu." Kwa kuwa tafsiri huzalishwa na mashine, sio tafsiri zote zitakuwa kamili. Jinsi nyaraka zaidi zilizotafsiriwa na wanadamu ambazo Google Tafsiri inaweza kutathmini katika lugha mahsusi, ndivyo ubora wa utafsiri utakuwa. Hii ndiyo maana usahihi wa utafsiri wakati mwingine utatofautiana kilugha.
Ni lugha gani ambazo Google Tafsiri hukubali?
Google Tafsiri kwa sasa hukubali:
Lugha za sasa za alfa ni:
Google Tafsiri hujaribu lugha zingine, zinazoitwa "lugha alfa," ambazo huenda zikawa na ubora wa utafsiri usioweza kutegemewa zaidi ya lugha zetu zinazokubaliwa. Daima tunafanya kazi ili kuunga mkono lugha zingine na tutazileta punde tu ubora wa utafsiri unapofikia viwango vyetu.
Ni nini ninachoweza kufanya ili kuboresha ubora wa Utafsiri?
Ukikabiliana na utafsiri ambao huonekani sawa, mara kwa mara Google Tafsiri itakua na matokeo mbadala yanayopatikana. Ili kuona hii, bofya kifungu kinachohusika. Wakati unapobofya utafsiri bora wa ziada, Google Tafsiri itajifunza kutoka kwa maoni yako na kuendelea kuboreshwa baada ya muda.
Unaweza pia kusaidia kuboresha ubora wa utafsiri kwa kutumia Zana za Mtafsiri za kutafsiri au kwa kupakia kumbukumbu zako za utafsiri kwenye Zana za Mtafsiri.
Unataka kujifunza zaidi?
Unaweza kusoma zaidi kuhusu visasisho vyetu vya karibuni kwenye Blogu ya Google Tafsiri na kuhusu miradi mingine ya Google ya utafitii kwenye tovuti ya Utafiti wa Google.
Kujifunza mengi kuhusu sayansi ya utafsiri wa mashine, angalia nyenzo hizi:
Bado unahitaji usaidizi? Tembelea tovuti yetu ya usaidizi hapa.
Tafsiri